Akiba Commercial Bank Plc imeendelea kujitoa si tu kuhudumia wateja wake bali pia kushiriki katika juhudi za kijamii wakati wa dharura na majanga, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kujenga jamii imara na yenye mshikamano.
Ameyasema hayo leo Novemba 17 ,2024 Jijini Dar es salaam na Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Tobha Nguvira, ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha maafa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kupokea msaada kutoka Akiba Commercial Bank walipokuja kutembelea eneo la ajali la jengo la biashara lililoporomoka Kariakoo, ajali iliyosababisha madhara makubwa, ikiwemo majeruhi, uharibifu wa mali na wengine kuangamia
"Tunashukuru sana Benki hii imetoa msaada wa katoni kadhaa za maji kwa ajili ya kusaidia timu ya uokozi inayofanya juhudi kubwa za kuokoa watu waliokumbwa na ajali hiyo mbaya na ya kusikitisha na wamekuja na Ujumbe wa Akiba Commercial Bank uliongozwa na wafanyakazi wa matawi ya Kariakoo pamoja na makao makuu , akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Bi. Dora Saria, na Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji, Dkt. Danford Muyango" ,amesema Dkt Nguvira.
Naye Kaimu Afisa Biashara Mkuu Dkt. Danford Muyango amesema Akiba Commercial imewaomba wateja wake ambao wameathirika na janga la kuporomoka gorofa kariakoo kufika kwenye matawi kutoa taarifa za athari walizopata kwani benki itatoa usaidizi wa tathmini wa kina kuhusu huduma za bima na kuanzisha utaratibu wa marejesho ya mikopo yao kulingana na hali yao .
Social Plugin