****
Kampuni ya BF SUMA Tanzania, inayojulikana kwa uzalishaji wa bidhaa zinazotibu magonjwa yasiyoambukiza, itaendesha semina muhimu itakayofanyika kesho Jumapili, Disemba 01, 2024, katika ukumbi wa mikutano wa Karena Hotel uliopo Manispaa ya Shinyanga.
Kiongozi wa BF SUMA, Juma Mwesigwa, amesema leo Novemba 30, 2024, kwamba semina hiyo, inayoitwa “AFYA YANGU, UCHUMI WANGU”, ni fursa muhimu kwa wananchi wa Shinyanga na maeneo jirani.
Semina hii itahusisha mada mbalimbali za biashara, afya, na tiba, ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, na bidhaa zinazotibu magonjwa hayo.
Mwesigwa ameeleza kuwa, semina hii ni ya kipekee kwani itahusisha madaktari wabobezi wa magonjwa yasiyoambukiza, na pia kutakuwa na vipimo vya bure kwa magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kisukari, saratani, presha, vidonda vya tumbo, magonjwa ya mifupa, pingili za mgongo, bawasiri, na mengineyo.
Aidha, washiriki wa semina hiyo watapata nafasi ya kupima afya zao bure, kwa hiari.
Juma Mwesigwa amefafanua kuwa bidhaa zinazozalishwa na BF SUMA ni bora kwa matumizi ya binadamu, na kwamba zimekuwa zikiingiza mabadiliko chanya katika afya ya watumiaji.
“Kampuni yetu inazalisha bidhaa bora ambazo ni tiba ya magonjwa yasiyoambukiza, na tunatarajia kuwa semina hii itakuwa na manufaa kwa watu wengi, hasa wale wanaohitaji msaada katika kutunza afya zao,” amesema.
Pia, Mwesigwa ametangaza kuwa BF SUMA imefungua ofisi mpya katika Manispaa ya Shinyanga, ndani ya jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), ghorofa ya nne.
Hii ni sehemu nyingine ya dhamira ya kampuni hiyo ya kupanua huduma zake kwa jamii.
Semina hiyo ni bure, na wananchi wote wanakaribishwa kushiriki. Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na kampuni ya BF SUMA kwa simu namba 0784 150 950.
Social Plugin