Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE LUCY MAYENGA APIGA KURA KUCHAGUA VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA

Mbunge viti maalum mkoa wa Shinyanga, Mh. Lucy Mayenga, leo tarehe 27 Novemba 2024 amepiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa. 

Mh. Mayenga alijitokeza kupiga kura katika eneo la Maganzo, wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, akionesha mfano mzuri wa kushiriki katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa. 

Ushiriki wake umeongeza hamasa kwa wananchi na kuhimiza umuhimu wa kujitokeza na kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya mitaa.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com