Chama chateua mwanachama mwingine achukua fomu na kurejesha muda huohuo, chadai mazishi ya mwanachama wao ni jumapili.
Na Adelinus Banenwa
Aliyekuwa amepitishwa na chama cha mapinduzi kugombea nafasi ya uwenyekiti wa kijiji cha Isanju kata ya Ilamba wilayani Bunda ndugu Tumaini Zakayo (60) amefariki usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza na radio Mazingira FM katibu wa siasa na uenezi CCM kata ya Ilamba ndugu Chigala Mshangi Maijo amesema ni kweli mwanachama wao amefariki katika hospitali ya Kibara alipofika kupata matibabu baada ya siku ya tarehe 31 Oct kudai anasumbuliwa na tumbo.
Chigala ameongeza kuwa ndugu Tumaini pamoja na wateule wengine wa chama cha mapinduzi katika kata hiyo walishiriki zoezi la urejeshaji wa fomu lililofanyika tarehe 30 Oct 2024 japo alitaja kuwa mgonjwa
Aidha Chigala ameongeza kuwa wao kama chama wamelazimika kuketi kikao cha dharula ili kuona wanawezaje kuiziba nafasi ya mgombea huyo aliyetangulia mbele ya haki ambapo tayari kama chama kimemteua mwanachama mwingine na tayari amechukua fomu ameijaza na tayari amekwisha irejesha kwa muda uliokuwa umepangwa na serikali.
Social Plugin