Hali hii inahatarisha usalama wa wateja na ustawi wa sekta ya kifedha, kwani majukwaa haya yanashindwa kutimiza matakwa ya Mwongozo wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili kwa mwaka 2024.
Hii inajumuisha uwazi katika utoaji wa huduma, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, na kulinda faragha ya taarifa binafsi za wateja.
Benki Kuu imefafanua kwamba majukwaa na programu tumizi zinazohusishwa na utoaji wa mikopo kidijitali ambazo hazijapata kibali kutoka kwa Benki Kuu haziruhusiwi kuendelea na shughuli hizo.
Hivyo, inatoa wito kwa umma na wadau wote kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kulinda haki za wateja na kuhakikisha sekta ya fedha inafanya kazi kwa uwazi na kwa maslahi ya wote.
Majukwaa na programu hizo ambazo hazina leseni hazitapata idhini ya kuendelea kutoa huduma za mikopo kidijitali, na Benki Kuu ya Tanzania inasisitiza kwamba watoa huduma hawa wanapaswa kusitisha huduma zao mara moja.
Benki Kuu inautahadharisha Umma kutojihusisha na Majukwaa na Progamu Tumizi “Applications” hizo.
Aidha, Benki Kuu inashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzifungia programu hizi ili kuepusha Umma kutumia huduma za fedha zisizokuwa na vibali vya Mamlaka husika. Benki Kuu imechapisha na itaendelea kuhuisha orodha ya watoa huduma walioidhinishwa kutoa huduma za mikopo katika tovuti yake.
Taarifa hii inapatikana kupitia tovuti ya Benki Kuu: https://www.bot.go.tz/Other/Orodha%20ya%20Watoa%20Huduma%20Ndogo%20za%20Fedha%20wa%20Daraja%20la%20Pili.pdf