Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wanapenda kuwajulisha wananchi na wadau wa habari kwamba zoezi la upigaji kura kwa washiriki wa Samia Kalamu Awards limeanza rasmi Novemba 11 na litaendelea hadi Novemba 20, 2024.
Zoezi hili linawahusisha wananchi ambao ndio walaji wa maudhui ya habari na ambao watakuwa na nafasi ya kuchangia asilimia 60 ya matokeo. Asilimia 40 ya alama zitakuwa zimetolewa na jopo la majaji kulingana na vigezo vya kitaaluma.
Huu ni wakati muhimu ambapo wananchi wanapata nafasi ya kutoa maoni yao kwa kupiga kura na kutoa maamuzi ya mwisho.
Wanahabari na vyombo vya habari vilivyokidhi vigezo vya kitaaluma vya uandishi wa habari za maendeleo ndivyo vitakavyoshiriki katika tuzo hizi. Makala 1,131 zilizowasilishwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwania Tuzo hizi, zimepitia mchakato wa uchambuzi wa kitaaluma na kazi 85 zilizokidhi vigezo zimewekwa kwenye tovuti ya www.samiaawards.tz na kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram (@samiakalamuawards), YouTube, na Facebook (Samia Kalamu Awards).
- Tembelea tovuti ya www.samiaawards.tz
- Fungua sehemu iliyoandikwa "Piga Kura"
- Chagua makundi ya Tuzo na namba ya mshiriki kwa kuangalia picha na kazi aliyochapisha
- Bofya Piga Kura ili kumchagua mshindi unayemtaka.
Kupiga Kura Kupitia Simu ya Kiganjani
- Nenda kwenye sehemu ya kutuma ujumbe wa kawaida (SMS)
- Andika neno “Kura”, acha nafasi, kisha weka namba ya mshiriki
- Tuma ujumbe kwenda namba 15200
- Utapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa kura yako imepokelewa.
Kaulimbiu ya Tuzo: "Uzalendo Ndio Ujanja"
Tuzo za Samia Kalamu Awards zimegawanywa katika makundi matatu makuu:
- Tuzo Maalumu za Kitaifa
- Tuzo za Vyombo vya Habari
- Tuzo za Kisekta
Lengo kuu la tuzo hizi ni kuhamasisha, kukuza na kupanua wigo wa uandishi wa habari za ndani kupitia vyombo vya habari vya asili na mitandaoni, ili kuchochea maendeleo, uwajibikaji, na kujenga taswira nzuri ya taifa letu.
Tunaomba Ushiriki Wenu!
Karibuni wananchi na wadau wa habari kushiriki kwa wingi katika mchakato huu wa upigaji kura ili kuhakikisha tunapata washindi wanaostahili.
Kwa maelezo zaidi, tembelea www.samiaawards.tz au wasiliana nasi kupitia namba +255716622200 na 0800008272
Kura Yako Ni Muhimu!
Jiunge na zoezi hili la kihistoria na changia kwenye ujenzi wa taifa letu kupitia uandishi wa habari bora.