TCAA YASHIRIKI MKUTANO WA WATAALAM WA LOGISTIKI NA USAFIRISHAJI NCHINI


Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi kutoka TCAA Bw. Daniel Malanga cha udhamini wa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
 ***

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Wizara ya Uchukuzi inaendelea na hatua ya kuweka Sheria mahususi ya usimamizi wa watalaam wa usafirishaji nchini.

Akizungumza jijini Dar es saalam Novemba 9, 2024 Prof. Mbarawa mara baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji amesema kuwa kwa sasa Wizara ya Uchukuzi inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Udhibiti Uchumi kutoka TCAA Bw. Daniel Malanga amesema Taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu kwa manufaa ya watanzania wote nchini.


Katika mkutano huo Bw. Malanga alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akiambatana na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Bw. Aristid Kanje.

Akiwasilisha mada ya Uhitaji wa Wataalam wa Lojistiki na Usafirishaji katika maendeleo ya Usafiri wa Anga, Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Bw.Aristid Kanje amesema kuwa ukuaji wa sekta ya Usafiri wa Anga unapelekea kuwa na uhitaji mkubwa wa wataalam wa lojistiki na usafirishaji. Na kuongeza kuwa sekta ya usafiri wa anga ina uhaba wa wataalam kama vile marubani, wahandisi wa kutengeneza ndege, waongoza ndege na kadhalika.


Bw. Kanje amesema kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kuwekeza kwenye mafunzo ya wataalam wa usafiri wa anga ili kukabiliana na mapungufu hayo.


Mkutano huo umehudhuriwa na taasisi zilizopo chini ya sekta ya uchukuzi pamoja na washiriki kutoka wizara ya Ujenzi, Tamisemi na vyuo vya elimu ya Juu.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wadau wa Logistiki na Usafirshaji wakati akifungua mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akizungumza namna wanavyoshirikiana na Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji hasa kwenye Usafiri wa Anga wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwasilisha mada kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na chuo cha CATC wakati wa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Logistiki na Usafirishaji wakifuatilia mada wakatiwa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa vyuo wakati wa mkutano wa Chama cha Watalaam wa Logistiki na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post