Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASMA MWINYI AAHIDI MISAADA YA MIUNDOMBINU KWA VETA PWANI, AWASISITIZA VIJANA KUTUMIA UJUZI KWA MAENDELEO

Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
******************

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi amewahimiza vijana wa VETA Pwani wanaohiti na wale wanaoendelea na masomo kutumia vizuri fursa ya ujuzi na kufanya bunifu zitakazoenda kutatua changamoto zilizoko katika jamii.

Alisema kwa kufanya hivyo itasaidia kuleta maana halisi ya kaulimbiu inayesema (Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa uchumi endelevu) akieleza kwamba ujuzi na bunifu ni nyezo muhimu katika taifa lolote linalohitaji maendeleo.

Wito huo ameutoa jana Novemba 7, 2024 wakati akihutubia katika mahafali ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Nitumie nafasi hii pia kutoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Serikali kwa kusaidia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji hasa wale wanaotoka kwenye mazingira magumu," alisema Asma.

Aidha katika Mahafali hayo, Asma aliahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya kwenda kusaidia kuboresha miundombinu ya kijifunzia katika chuo hicho.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Pwani Clara Kibodya ameziomba asasi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali kuendelea kufadhili vijana walio katika mazingira magumu kwa kutambua mahitaji yao na kisha kuwapeleka VETA ili kupatiwa mafunzo elimu ya ujasiriamali.

Alisema mafunzo hayo yatawatengenezea fursa za kujiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi na kwamba hiyo itapunguza wimbi la vijana wasio na ajira.

"Mafunzo ya VETA huendeshwa kwa mfumo wa ufundi mahiri ambao unalenga na kuzingatia ujuzi unaoendana na soko la ajira. Muundo mzima wa mafunzo humpatia mwanafunzi mazoezi mengi ya vitendo, elimu ya nadharia na tabia, sambamba na mafunzo viwandani, hivyo yatasaidia vijana wetu kutumia ujuzi watakaupata kujitengenezea kipato," alisema Clara.

Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akizungumza katika ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akizungumza katika ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akizungumza katika ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akizungumza katika ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akizungumza katika ya 14 ya Chuo cha VETA Pwani, ambapo alikuwa mgeni rasmi.Mahafali hayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akipata picha ya pamoja na wahitimu wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akipokea zawadi ya nguo kutoka kwa wanafunzi wa Chuo Cha VETA Pwani kwenye Mahafali 14 ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Asma Mwinyi Foundation (AMF) Asma Mwinyi akitazama vifaa maalumu vya kujifunzia wanafunzi wa Chuo Cha VETA Pwani wakati wa Mahafali 14 ya VETA Pwani ambayo yamefanyika leo Novemba 7, 2024 Kibaha mkoani Pwani.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com