ATEMBEA UCHI AKIPINGA SHERIA YA KUVAA HIJAB


Wanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito kwa mamlaka nchini Iran kumwachilia mwanamke aliyekuwa kizuizini baada ya kuvua nguo chuo kikuu, katika kile walichosema ni kupinga sheria za lazima za kuvaa hijab.

Video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi ikimuonyesha mwanamke huyo akiwa amevaa nguo ya ndani huku ameketi kwenye ngazi, kisha akatembea kwa utulivu kwenye barabara ya Tawi la Sayansi na Utafiti la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Azad mjini Tehran.

Katika video ya pili, mwanamke huyo anaonekana kuvua chupi yake. Muda mfupi baadaye, maafisa waliovalia kiraia wanaonekana wakimshikilia kwa nguvu na kumsukuma ndani ya gari.

Chuo Kikuu cha Azad kilisema mwanamke huyo alikuwa na “matatizo ya akili” na aamepelekwa “hospitali ya matatizo ya akili”.

Raia wengi wa Iran kwenye mitandao ya kijamii walitilia shaka madai hayo na kueleza vitendo vyake kama sehemu ya vuguvugu linalojulikana kama “Woman, Life, Freedom” ambalo limeshuhudia wanawake wengi wakipinga hadharani sheria zinazowataka kufunika nywele zao na kuvaa nguo ndefu zisizowabana.


Zaidi ya watu 500 waliripotiwa kuuawa wakati wa maandamano ya nchi nzima yaliyozuka miaka miwili iliyopita baada ya mwanamke wa Kikurdi, Mahsa Amini, kufariki akiwa mikononi mwa polisi baada ya kuzuiliwa kwa kutovaa hijabu “vizuri”.


Ilisema kichwa cha mwanamke huyo kiligonga mlango au fremu ya gari la maafisa waliokuwa wamevalia kiraia wakati akizuiliwa na kusababisha kuvuja damu na kupelekwa kusikojulikana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post