Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekutana na Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, Katibu Mkuu wa Convention for the Renewal of the Comoros (CRC), chama tawala nchini Comoro.
Mazungumzo hayo ya pande mbili, yaliyohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya vyama hivyo, serikali na nchi hizo mbili kwa ujumla, yalifanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Novemba 2024.
Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Katibu wa Rais wa Comoro, yupo nchini kwa ziara ya kikazi inayoendelea kuanzia tarehe 2 hadi 5 Novemba 2024.
Social Plugin