Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.
Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi.
Aidha Katika vitongoji 1849 vya Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.
Social Plugin