Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ENGONGA ATINGISHA MITANDAO VIDEO 400 ZA NGONO AKIFANYA MAPENZI NA WAKE ZA WATU OFISINI



Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa shirika la ANIF la nchini Equatorial Guinea, Afrika bw. Baltasar Ebang Engonga amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kusambaa kwa video za ngono 400 zikimuonesha akifanya mapenzi na wanawake tofauti tofauti wakiwemo wake wa mawaziri, mke wa mdogo wake, mtoto wa mkuu wa polisi, mke wa mchungaji wake, mke wa mjomba wake aliyekuwa mjamzito, wake wa marafiki zake pamoja na wake wa viongozi wengine wa serikali. 

Video hizo zimeonekana baada ya Baltasar kushutukiwa na wafanyakazi wenzake kwamba anahusika na masuala ya rushwa, akawekewa mtego na baadaye kukamatwa ambapo maafisa wa taasisi hiyo, walienda kupekua nyumbani kwake, wakitafuta ushahidi wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili, baada ya katika ukaguzi huo ndipo walipokuta laptop iliyokuwa ikitumiwa na Baltasar, ikiwa na video nyingi akiwa na wanawake tofauti, wakifanya mapenzi.

Mamia ya kanda za ngono zinazomhusisha mtumishi wa serikali wa ngazi ya juu wa Equatorial Guinea pamoja na wake za watu zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha mamlaka kujaribu kuzuia kuenea kwa video hizo.

Katika video hizo mkurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha (ANIF), Baltasar Ebang Engonga, anaonekana akiwa na wanawake mbalimbali - wakiwemo wake za maafisa mashuhuri -ofisini kwake katika wizara ya fedha.

Siku ya Jumatatu, makamu wa rais wa nchi hiyo Teodoro Nguema Obiang Mangue alitangaza kwenye X kwamba serikali itaamuru "kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi wote wa umma ambao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi katika ofisi za wizara, kwani hii ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za maadili na sheria ya maadili ya umma".

Si mara ya kwanza kwa kanda za ngono zinazohusisha watumishi wa umma kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini suala hilo limevuma kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea kutokana na sifa mbaya za viongozi waliohusika.

Wiki iliyopita, Obiang alisema kuwa ametoa notisi ya saa 24 kwa wizara ya mawasiliano ya Guinea ya Ikweta, mdhibiti na makampuni ya simu "kuzuia usambazaji wa video za ngono ambazo zimejaa mitandao ya kijamii nchini Equatorial Guinea".

"Kama serikali, hatuwezi kuendelea kuona familia zikiharibiwa," makamu wa rais anayehusika na ulinzi na usalama alisema.

Kulingana na akaunti zilizosambazwa kwa mara ya kwanza na vikundi vya Whatsapp na kisha kuwekwa kwenye Facebook, Instagram, TikTok na X, Engonga alipiga zaidi ya video 400 za ngono ofisini kwake.

Kanda hizo za ngono zilivujishwa kwenye mitandao ya kijamii wakati ambapo alikuwa amewekwa rumande katika gereza maarufu la Black Beach la Malabo katika kesi ya ubadhirifu wa fedha za umma, kulingana na kituo cha televisheni cha serikali TVGE.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Equatorial Guinea Anatolio Nzang Nguema, aliihakikishia TVGE kwamba ikiwa uchunguzi wa kimatibabu utabaini kuwa Ebang Engonga "alikuwa na ugonjwa wa zinaa" atafunguliwa mashtaka kwa kosa dhidi ya "afya ya umma".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com