WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA , WENYEVITI PRESS CLUBS WAJENGEWA UELEWA KUHUSU MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI

Katika hatua muhimu ya kuongeza ufanisi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amefungua kikao kazi cha waandishi wa habari kilicholenga kutoa elimu na uelewa wa kina kuhusu utekelezaji wa mpango huu unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Kikao hiki cha siku mbili kilichohudhuriwa pia na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu, kimeandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) kwa ushirikiano na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Katika hotuba yake, akifungua kikao hicho leo, Alhamisi, Novemba 7, 2024, Mhe. Macha amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kupitia mpango huu, ambao unalenga kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya kaya maskini.

Amesema ufanisi wa mpango huo hautegemei tu sera nzuri bali pia ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali, akiwemo vyombo vya habari.

Mfuko wa TASAF, kupitia mpango huu, unajizatiti katika kuhakikisha kuwa kaya maskini zinapata msaada wa kifedha na ushauri wa kiuchumi, ili kuwawezesha kujikimu kimaisha.

Mkurugenzi wa Mifumo na Mawasiliano TASAF , Japhet Boaz amesema wanawajengea uelewa waandishi wa habari kwa sababu ni kundi muhimu linapaswa kuwa na uelewa wa kutosha kwa ajili ya kutoa taarifa sahihi na za kina, ili jamii iweze kuelewa na kuchukua hatua zinazohitajika ili kunufaika na mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kilichofanyika akizungumza leo Alhamisi Novemba 7,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkurugenzi wa Mifumo na Mawasiliano TASAF , Japhet Boaz akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga  na Wenyeviti wa Klabu za Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Tabora, Geita na Simiyu kuhusu utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post