AJALI YA HIACE, FUSO YAUA WATU 14 TABORA


Watu 14 wamepoteza maisha na wengine tisa kujeruhiwa baada ya ajali ya gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.562 DGG kugongana na lori lenye namba T.361 CSB kwenye barabara ya Itobo - Bukene, katika kijiji cha Mwasengo, wilayani Nzega, mkoani Tabora.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, amethibitisha ajali hiyo iliyotokea Novemba 07, 2024 saa mbili asubuhi. Watu kumi na wanne wamefariki, wakiwemo wanaume wanane, wanawake wanne, na watoto wawili. Majeruhi tisa wapo hospitalini kwa matibabu.

Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Hiace, aliyekuwa akijaribu kulipita lori na kushindwa kulimudu, na hivyo kuligonga lori hilo upande wa kulia na kuingia chini ya uvungu wake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa, Richard Abwao, amesema Dereva wa Hiace bado hajafahamika kwa kuwa alikimbia baada ya ajali hiyo, ambayo chanzo chake kimebainika kuwa ni uzembe wa dereva huyo wa Hiace, alipokuwa akijaribu kulipita Fuso na kuligonga kwa nyuma

Jeshi la Polisi linaendelea na ukaguzi wa magari yanayohatarisha usalama kwa mwendokasi.

 Abiria pia wametakiwa kupaza sauti kwa dereva anayeendesha kwa njia hatarishi. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega, na miili tisa imetambuliwa na ndugu. 

Majeruhi wawili wanapatiwa matibabu Nzega, huku saba wakipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Nkinga.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post