BoT YATOA POLE AJALI YA GHOROFA KUPOROMOKA DAR, ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDELEA

 
Benki Kuu ya Tanzania imetoa pole kwa wananchi waliojeruhiwa na kupoteza maisha katika tulio la kuporomoka kwa jengo Kariakoo ambapo idadi ya watu waliopoteza maisha yao Jumamosi ya Novemba 16, 2024 kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Wakati jitihada za kuwaokoa Watu waliofunikwa na Vifusi Kariakoo zinaendelea, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga amesema mawasiliano yanaendelea na baadhi ya waliokwama, wanapatiwa huduma muhimu, huku akiahidi watahakikisha wanatolewa wakiwa wazima

Jenerali Masunga amesema “Shughuli ya uokoaji imeendelea mfululizo tangu jana. Tumeweza kuwasiliana na baadhi ya waliopo chini ya kifusi, na kwa sasa tumewapatia maji, glucose, na kuwahakikishia vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko hapa kuhakikisha wanatoka salama. Tuna faraja kubwa kwamba huduma hizo zimewafikia wakiwa salama ndani ya eneo hilo.”

Jengo hilo la ghorofa 4 liliporomoka Novemba 16, 2024 asubuhi katika Soko Kuu la Kariakoo, ambapo hadi sasa Watu Watano wameripotiwa kufariki, huku majeruhi 70 wakiokolewa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post