Wakati jitihada za kuwaokoa Watu waliofunikwa na Vifusi Kariakoo zinaendelea, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga amesema mawasiliano yanaendelea na baadhi ya waliokwama, wanapatiwa huduma muhimu, huku akiahidi watahakikisha wanatolewa wakiwa wazima
Jenerali Masunga amesema “Shughuli ya uokoaji imeendelea mfululizo tangu jana. Tumeweza kuwasiliana na baadhi ya waliopo chini ya kifusi, na kwa sasa tumewapatia maji, glucose, na kuwahakikishia vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko hapa kuhakikisha wanatoka salama. Tuna faraja kubwa kwamba huduma hizo zimewafikia wakiwa salama ndani ya eneo hilo.”
Jengo hilo la ghorofa 4 liliporomoka Novemba 16, 2024 asubuhi katika Soko Kuu la Kariakoo, ambapo hadi sasa Watu Watano wameripotiwa kufariki, huku majeruhi 70 wakiokolewa
Social Plugin