Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, amezindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’ ambapo amekabidhi vifaa vya michezo kwa Timu 12 zinazoshiriki huku akiahidi kutoa zawadi nono kwa washindi kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tano.
Katika hafla hiyo, iliyofanyika leo Jumamosi Novemba 2,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Kitangili United ilipata ushindi dhidi ya Mwadui United kwa bao 2-0, huku Upongoji Stars ikishinda 1-0 dhidi ya Young Stars.
Mhandisi Jumbe, mzaliwa wa Mtaa wa Majengo, Mjini Shinyanga amesema Mashindano ya mwaka huu yana mvuto wa aina yake hivyo mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya Ng’ombe, Kilo 200 za mchele , Kreti nne za soda pamoja na kitita cha shilingi Milioni tatu, Washindi wa pili na wa tatu pia wataondoka na zawadi nzuri, huku washindi wa nne na wa tano wakipata mbuzi wawili,mchele kilo 100 na shilingi 200,000 kila mmoja.
Mhandisi Jumbe amekumbuka jinsi alivyoshiriki mwaka jana, akichangia vifaa vya michezo na zawadi kwa washindi. "Mwaka jana 2023, mshindi wa kwanza alikabidhiwa ng'ombe na kilo 200 za mchele, mshindi wa pili mbuzi wawili na kilo 100 za mchele," Kwa mwaka huu, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wote watapata ng'ombe na mchele, tofauti ni katika zawadi za fedha..Lakini pia kila timu itapata shilingi 200,000 kwa ajili ya maji."
"Kwa mwaka huu Mshindi wa kwanza hadi wa tatu wote watapata ng’ombe, kilo 200 za mchele, Kreti nne za soda. Tofauti yao sasa mshindi wa kwanza atapata shilingi Milioni tatu, mshindi wa pili shilingi milioni mbili, na mshindi wa tatu shilingi milioni moja. Lakini mshindi wanne na wa tano asitoke kinyonge ahamasike atapata mbuzi wawili, kilo 100 za mchele na soda pamoja shilingi 200,000 kwa mshindi wa nne na wa tano”,ameeleza Jumbe.
Kwa heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mhandisi Jumbe amesisitiza umuhimu wa kuongeza jina la Rais kwenye mashindano hayo. "Rais Samia ni mdau mkubwa wa michezo, na amekuwa akitoa zawadi kwenye michuano ya kimataifa. Kwa heshima yake, ningependa jina lake pia lionekane kwenye mashindano hay badala ya jina la Jumbe. Kwa heshima yake na kwa muda ambao amekuwa Rais ametufanyia mambo makubwa ningependa yaitwe DR. SAMIA – JUMBE CUP”,ameongeza Mhandisi Jumbe.
Pia amewahamasisha wachezaji kuonyesha nidhamu na ushindani mzuri bila kuleta majeraha.
"Mchezo wa mpira siyo wa kuwatenganisha watu, bali ni wa kuwaunganisha. Shinyanga ina historia kubwa ya mpira wa miguu nchini kwa hiyo tunataka turudishe mpira wetu Shinyanga lazima tulete mabadiliko kuanzia ngazi ya chini hadi juu”,amesema.
"Tuendelee kumuomba Mungu ili mwaka ujao nipate nafasi nzuri ya kujipanga zaidi na kuboresha uwezo wetu. Nitatumia pia uhusiano wangu kuunganisha wachezaji wenye vipaji na fursa za kufanya majaribio kwenye timu kubwa",ameongeza.
Mbali na kuhamasisha mashindano hayo, Mhandisi Jumbe pia ameahidi kusaidia timu zinazoshiriki Ligi ya Mkoa kwa kutoa shilingi milioni moja kwa kila timu. Timu hizo ni Katunda FC, Boko FC na Mshikamano Shy FC, ambazo zipo katika Wilaya ya Shinyanga huku akiwahakikishia waamuzi wa mchezo vifaa vya michezo zikiwemo Jezi.
Aidha, amewakumbusha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024 akiwaomba wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi kwenye maeneo yao kwa sababu uchaguzi ni muhimu sana.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga , Joseph Assey, na Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza, wamemshukuru Mhandisi Jumbe kwa udhamini wa Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya, wakisema kwamba utasaidia kuinua vipaji vya wana michezo wanaoshiriki kwenye ligi hiyo.
Nazo timu zinazoshiriki mashindano hayo zimemshukuru Mhandisi Jumbe kwa msaada mkubwa alioutoa kwao katika kuhakikisha timu zinapata vifaa vya michezo na zawadi ambazo zinawaongezea motisha ambapo kwa upendo na kujitolea kwake, amedhihirisha kwamba anajali maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu katika Wilaya ya Shinyanga.
Timu 12 zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga 'Dr. Samia - Jumbe Cup' ni Lwambogo FC, Upongoji FC, Original FC, Upongoji Star, Qatar Fc, Mwadui United, Kitangili United, Rangers FC, Magereza FC, Kambarage Market na Waha FC.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akizungumza leo Jumamosi Novemba 2,2024 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’ yakishirikisha Timu 12 huku akiahidi kutoa zawadi nono kwa washindi kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tano. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’ yakishirikisha Timu 12

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti akisalimiana na wachezaji wa timu ya Upongoji Stars wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti akisalimiana na Waamuzi wa Mpira wa Miguu wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti akisalimiana na wachezaji wa timu ya Young Stars ya Tinde wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’
Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa (mwenye tisheti ya bluu) akiwa katika uwanja wa CCM Kambarage alipowasili kuzindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu 12 wakati akizindua rasmi mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’
Sehemu ya vifaa vya michezo

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga Joseph Assey (kushoto) akiteta jambo na Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa
Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga Joseph Assey akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu 12 zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama "DR. SAMIA – JUMBE CUP’

Picha za kumbukumbu na Mhandisi James Jumbe Wiswa

Picha za kumbukumbu na Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa
Wadau wa michezo wakifuatilia mechi
Wadau wa michezo wakifuatilia mechi
Young Stars kutoka Tinde wakipiga ya kumbukumbu
Upongoji Stars wa Manispaa ya Shinyanga wakijipatia bao la ushindi dhidi ya Young Stars ya Tinde Halmashauri ya Shinyanga
Mchezo kati ya Upongoji Stars (jezi ya bluu) na Young Stars ukiendelea.

MC Mzungu Mweusi akitangaza mechi
Upongoji Stars wakipiga picha ya pamoja
Mchezo kati ya Kitangili United na Mwadui United (jezi za kijivu) ukiendelea

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog