HAYA HAPA MAJINA YA MAJERUHI AJALI YA GHOROFA KUPOROMOKA KARIAKOO
Saturday, November 16, 2024
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha mtu mmoja na wengine 28 kuokolewa wakiwa wamejeruhiwa katika ajali ya kuporomoka kwa ghorofa iliyotokea asubuhi ya leo, Novemba 16 Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye eneo la ajali, Waziri Mkuu amesema serikali kupitia kwa vikosi vya uokoaji itahakikisha shughuli hiyo inafanyika mpaka watu wote waliokuwepo kwenye jengo hilo wakati wa ajali wanathibitika iwapo wako hai au wamefariki.
Nacho kikosi cha zimamoto na uokoaji kimesema kuwa kinaendelea na juhudi za kuwaokoa watu walionaswa kwenye vifusi ikiwa ni pamoja na kuwapelekea hewa ya oksijeni kupitia mipira maalumu ili kuwasaidia kupata hewa safi wakisubiri uokozi.
Shughuli ya uokoaji inaendelea katika kifusi cha ghorofa hilo lililokuw akatika makutano ya mtaa wa Kongo na Mchikichi.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin