Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LISSU ATAJA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI CHADEMA KATIKA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 
Kiongozi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameweka wazi changamoto kubwa ambazo chama hicho kinakutana nazo katika maandalizi ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024

Katika mahojiano na Mwanahabari Chief Odemba ameonyesha jinsi chama hicho kinavyokumbana na changamoto kubwa katika kukusanya rasilimali fedha, watu, na vifaa. 

Hali hii inadhihirisha wazi kwamba Chadema hawana uwezo wa kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya uchaguzi.

Ingawa Chadema wanakiri sasa kwamba hawawezi kukusanya fedha, rasilimali, au watu wa kutosha kuendesha kampeni yenye mafanikio, ni wazi kuwa watakapopata matokeo ya uchaguzi, wataendelea kudai kwamba uchaguzi huo umeporwa kwao. 

Hii inaonesha jinsi Chadema wanavyoshindwa kukubali ukweli na badala yake wanageuza kila kipande cha kushindwa kuwa kisingizio cha kudai udanganyifu. Wananchi wanapaswa kuangalia kwa makini na kuelewa kwamba Chadema wanajenga mazingira ya kutafuta huruma badala ya kujiandaa kwa ushindani wa haki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com