Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup", yamehitimishwa kwa kishindo kikubwa baada ya Timu ya Rangers FC kuibuka mabingwa, wakiishinda Original FC kwa bao 3-2 katika fainali kali iliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Rangers FC wameonesha furaha kubwa wakiondoka na zawadi nono kutoka kwa mdhamini Mkuu wa mashindano hayo, Mhandisi James Jumbe Wiswa, ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini.
Zawadi za bingwa zimejumuisha Kombe, Ng’ombe, Kilo 200 za mchele, Kreti nne za soda, na Milioni tatu kwa timu ambapo Ushindi huu ni uthibitisho wa juhudi na nidhamu ya timu hiyo, iliyopambana vikali hadi dakika za mwisho.
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Original FC, ambao walikosa ubingwa kwa kufungwa kwa bao 3-2, wameondoka na zawadi ya Ng'ombe, Kilo 200 za mchele, Kreti nne za soda, pamoja na Shilingi Milioni mbili huku Timu ya Upongoji Sports Club, wakiwa washindi wa tatu, wakijivunia zawadi ya Ng’ombe, Kilo 200 za mchele, Kreti nne za soda, na Shilingi Milioni moja.
Mshindi wa nne Kitangili United FC na mshindi wa tano Upongoji Stars FC wameondoka na kifuta jasho cha mbuzi wawili ,mchele kilo 200 na shilingi 200,000 kila mmoja.
Kando na zawadi za timu, mashindano haya yametoa zawadi za kipekee kwa wachezaji na wadau waliotamba uwanjani akiwemo Mfungaji Bora: Athumani Kwegu kutoka Rangers FC aliyeonyesha ustadi wa kipekee kwa kufunga mabao muhimu na Mchezaji Bora Chipukizi: Mohamed Nassoro kutoka Kitangili FC aliyeibuka mchezaji chipukizi bora.
Zawadi zingine zimeenda kwa Golikipa Bora: Mathias Bakari kutoka Kitangili FC aliyekua kipenzi cha wengi, Kocha Bora: Dionizi Charles wa Original FC aliyekubalika kwa uongozi wake makini , Mwamuzi Bora: John Tanganyika aliyejivunia zawadi ya mwamuzi bora, akiendesha michezo kwa usahihi na ufanisi na Timu yenye Nidhamu Bora, Young Stars FC wakiondoka na zawadi ya timu yenye nidhamu bora.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi, Mhandisi James Jumbe amewashukuru wadau wa michezo, akisisitiza kuwa mashindano ya mwaka huu yameonyesha mvuto mkubwa na kwa hakika yalistahili kuitwa "Dr. Samia – Jumbe Cup", kwa heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya michezo nchini.
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa
“Ni furaha yangu kuona michuano hii ikifanya vizuri na kutoa nafasi kwa vijana wetu kuonyesha vipaji vyao. Ninaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo kwa kupitia mpango wa Goli la Mama, na natumai kila mmoja atajitokeza kuunga mkono timu za soka za Shinyanga. Tunataka kurudisha heshima ya Mkoa wa Shinyanga katika soka,” amesema Mhandisi Jumbe, ambaye pia ni mzaliwa wa Majengo Mjini Shinyanga.
Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga, Joseph Assey, Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza, na Diwani wa Kata ya Kambarage, Mhe. Hassan Mwendapole, wametoa pongezi za dhati kwa Mhandisi Jumbe kwa kudhamini mashindano haya na kuimarisha michezo katika mkoa wa Shinyanga.
Wamesema Mhandisi Jumbe ameleta mapinduzi makubwa katika michezo ya Shinyanga na kupitia mashindano hayo Wana Shinyanga wamepata fursa ya kuona vipaji vya vijana, matamanio makubwa yakiwa ni kuendelea kuwa na mafanikio zaidi.
Kumalizika kwa mashindano haya, mkoa wa Shinyanga umeonesha kuwa ni hazina ya wachezaji wenye vipaji, na kwamba soka katika eneo hili lina mustakabali mzuri.
Mashindano haya yamefungua milango ya ajira na fursa nyingi kwa vijana, na inatarajiwa Shinyanga itakuwa kitovu cha maendeleo ya soka nchini.
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup" katika uwanja wa CCM Kambarage Novemba 28,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"katika uwanja wa CCM Kambarage Novemba 28,2024
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Timu ya Rangers FC wakifurahia Ubingwa wa Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi Kombe kwa Timu ya Rangers FC kwa kuibuka washindi wa kwanza Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"

Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi zawadi ya shilingi Milioni tatu kwa Timu ya Rangers FC kwa kuibuka washindi wa kwanza Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Kombe la Ushindi Timu ya Rangers FC washindi wa kwanza Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi zawadi ya shilingi Milioni mbili kwa Timu ya Original FC kwa kuibuka washindi wa pili Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi zawadi ya shilingi Milioni 1 kwa Timu ya Upongoji Sports Club kwa kuibuka washindi wa tatu Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi zawadi kwa Timu ya Kitangili United FC Ckwa kuibuka washindi wa nne Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akikabidhi zawadi kwa Timu ya Upongoji Stars Fc kwa kuibuka washindi wa tano Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Ng'ombe na mbuzi zawadi kwa washindi Msanii Ng'wana Kang'wa akitoa burudani
Msanii Ng'wana Kang'wa na wanenguaji wake wakitoa burudani
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe akiendelea kukabidhi zawadi

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga, Joseph Assey akikabidhi cheti cha shukrani Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe aliyedhamini Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, maarufu kama "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Afisa Michezo wa Manispaa ya Shinyanga, Anord Rukiza akizungumza
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga, Joseph Assey akizungumza Diwani wa Kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akizungumza
Rangers FC
Original FC
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, "Dr. Samia – Jumbe Cup"

Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc vs Original FC ikiendelea Mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, "Dr. Samia – Jumbe Cup"
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC ikiendelea
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC ikiendelea
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC ikiendelea
Mdau wa michezo Jackline Isaro akifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Wadau wakifuatilia mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC ikiendelea
Mechi ya fainali kati ya Rangers Fc na Original FC ikiendelea
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akisalimiana na wachezaji wa Original FC
Mdau wa Michezo Mhandisi James Jumbe Wiswa akisalimiana na wachezaji wa Rangers Fc
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin