Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC), amezindua Rasmi Kampeni za Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga,ambao watapeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa,ni kutafuta viongozi wa Vijiji,Mitaa,Vitongoji na wajumbe, ambao watadumu kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2029.
Uzinduzi wa Kampeni hizo za CCM mkoani Shinyanga,umefanyika leo Novemba 20,2024 katika Kata ya Bubiki wilayani Kishapu.
Bashe akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hizo, amesema Mkoa wa Shinyanga una Mitaa 90,Vijiji 506 na Vitongoji 2,703, na kwamba CCM imeweka wagombea wengi kuliko vyama vya upinzani,ambao wenyewe wameweka wagombea asilimia 23, na hivyo kusababisha CCM kuwa tayari imeshashinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa asilimia 77.
Amewataka wananchi siku ya kupiga kura Novemba 27, wajitokeze kwa wingi kupiga kura, na wawachague wagombea wote wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambao ndiyo watawaletea maendeleo.
“Leo tunazindua kampeni za uchaguzi hapa mkoani Shinyanga,huku CCM tukiwa tayari tumeshashinda kwa asilimia 77,”amesema Bashe.
Aidha,amewaahidi wananchi wa Bubiki kuwa Serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwamba kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2025, watapata huduma ya majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria.
Pia, amesema serikali itaendelea kuboresha kilimo cha zao la Pamba ili kumnyanyua mkulima kiuchumi, kwa kumpatia Mbegu bure za Pamba na Madawa, pamoja na kuajiri maofisa ugani 2,000, na kwamba kila kijiji kitakuwa na Ofisa Kilimo na atakuwa na Pikipiki.
Amesema mbali na utoaji huo wa Ruzuku za kilimo, Pia bei ya Pamba itaimarishwa zaidi, na kwamba itakuwa ikibandikwa kwa kila AMCOS, na Mkulima atakuwa akipewa risiti muda wa saa 9 mchana, ili apate malipo halali kulingana na bei husika, sababu bei ya pamba itakuwa ikibadilika badilika.
Katika hatua nyingine, amesema Serikali itafanya uchunguzi wa kina juu ya mtandao mzima wa watu ambao walihusika kuiba Mbegu za Pamba, katika Amcos ya kijiji cha Mwamishoni kata hiyo ya Bubiki, ili kupata mtandao mzima na wapi walikuwa wakipeleka kuuza mbegu hizo ambazo zilikuwa tayari na madawa.
Amesema uchunguzi utakapokamilika, na kubaini Ginery ambazo zilikuwa zikipelekewa kuuziwa mbegu hizo za Pamba za wizi, zitafungiwa kutofanya biashara tena ya kununua Pamba wala kukamua mafuta yatokanayo na mbegu za pamba.
“Watu hawa waliohusika na wizi wa mbegu wapo kwenye mikono ya dola, na kuiba mbegu hizi ni kosa la uhujumu uchumi,na watu hawa ni wauwaji sababu mbegu zilikuwa na madawa,kukamua mafuta na kuuzia watu au kutumika katika mashudu ya ng’ombe wa maziwa ni kulisha sumu wananchi,”amesema Bashe.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema CCM itashinda kwa kishindo, huku akimpongeza Waziri Bashe kwa kumshauri vizuri Rais Samia, na sasa ametoa Matrekta 24 wilayani humo, ambayo yatampunguzi gharama mkulima katika kilimo, na kwamba hekali moja ya shamba atakuwa akilimiwa kwa Sh.35,000 kutoka Sh.70,000.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu,amewataka wananchi kwamba katika uchaguzi huo wa Serikali za mitaa, wawapigie kura wagombea wa CCM, nawasije kuchaganya na wagombea wa upinzani, ili kuwepo na myonyoro wa uongozi thabiti na wenye kuwaletea maendeleo kuanzia ngazi ya chini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema CCM katika Mkoa wa Shinyanga wamejipanga vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na watashinda kwa kishindo, sababu ya kumpatia zawadi Rais Samia Suluhu Hassan, kutokana na maendeleo makubwa ambayo ameyafanya mkoani humo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza wakati wa kuzindua kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akinadi wagombea wa CCM Kata ya Bubiki ambao wanapeperusha Bendera kwenye uchaguzi wa Serikali ya Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwaapisha wagombea wa CCM Kata ya Bubiki ambao ni wenyeviti wa vijiji,vitongoji na wajumbe ambao watapeperusha bendera kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika novemba 27,2024.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM.
Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM
Mbunge wa Vitimaalum Lucy Mayenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Diwani wa Bubiki James Kasomi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Uzinduzi wa kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika Kata ya Bubiki wilayani Kishapu.