Na Regina Ndumbaro, Ruvuma
Kanali Ahmed Abbas Ahmed, aliyekuwa mgeni rasmia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Kitaifa, yaliyofanyika katika Viwanja vya Majimaji, Manispaa ya Songea, Novemba 25,2024 amesema kuwa licha ya takwimu kuonyesha maambukizi ya Virusi vya VVU yameshuka, bado kuna haja ya kuendelea na juhudi za kuzuia maambukizi hayo ili kufikia malengo ya kutokomeza kabisa ugonjwa wa UKIMWI.
Akizungumza katika ufunguzi huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, na viongozi wa kidini, Kanali Ahmed Abbas Ahmed amebainisha kuwa maambukizi ya Virusi vya VVU katika mkoa wa Ruvuma bado yapo hivyo kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia mikakati ya afya ili kupambana na maambukizi hayo.
Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kitafanyika tarehe Mosi Desemba 2024, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.
Social Plugin