***
Na James Salvatory
Kampeni hiyo inalenga kutoa
vifurushi vya simu bora na nafuu, ikiwa ni pamoja na Dakika, Intaneti, na
Ujumbe Mfupi (SMS) vilivyoboreshwa, kwa ajili ya kuwafaidi wateja wao katika
maeneo yote ya nchi, mjini na vijijini.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es
Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL,
Vedastus Mwita, amesema kuwa lengo kuu la kampeni ya “WALETE” ni kuwafikia
Watanzania wote na kutoa huduma zinazokidhi mahitaji yao ya mawasiliano, hasa
katika nyakati hizi za teknolojia ya kidijitali.
Aidha, Mwita amesema kupitia kampeni
ya “WALETE,” kumefanyika maboresho kwa kuongeza BONUS kubwa kwenye vifurushi
vya mawasiliano, ikiwemo Dakika, SMS, na Kifurushi cha Jiachie Xtraa, ambacho
kinampa mteja fursa ya kupata muda wa kutosha wa kupiga kwenda mitandao yote na
ujumbe mfupi (SMS) kwa gharama nafuu na bila ukomo wa muda.
Kifurushi kingine ni cha T-Connect
Plus, ambacho kimeongezea muda wa maongezi, ambapo mteja atanunua kifurushi
hicho na kupata faida ya Intaneti, ujumbe mfupi (SMS), pamoja na muda wa
maongezi ambao ataweza kupiga kwenda mitandao yote.
Katika hatua nyingine, Mwita amesema
kuwa kutokana na kukua kwa matumizi ya kidijitali, wameboresha upatikanaji wa
vocha kwa njia ya kidijitali hivyo, hivi sasa mteja anaweza kupata vocha
kupitia Mawakala wa T-RUSHA.
Aidha, vocha pia zinapatikana kwa
njia ya kidijitali kupitia T-Pesa, kwenye Benki ya CRDB, NMB, Selcom, na
mitandao mingine ya simu. Vilevile, vocha za kukwangua bado zinapatikana kwa
mawakala waliopo maeneo mbalimbali na kwenye maduka yao.
Akizungumzia kuhusu kifurushi cha
Bufee Tena, ambacho kimeboreshwa zaidi na kwa gharama nafuu, Mwita amesema
kifurushi hicho kinampa mteja uhuru wa kuchagua kiwango anachotaka, iwe Dakika,
SMS, au Data, kulingana na mahitaji yake.
Kwa upande wake, balozi wa kampeni
ya “WALETE,” Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo, ambaye pia ni mtangazaji
wa Wasafi FM na mwanamuziki, amesema kuwa TTCL kwenye upande wa Intaneti iko
bora zaidi na indipo inapoonesha ukubwa na ubora kwenye kumfanya Mtanzania
kuperuzi kwa haraka zaidi.
“Mtandao wa TTCL kwenye upande wa Intaneti hapo ndipo tutakapoonyeshana ukubwa, kwani ndio wapo bora zaidi kwenye kumfanya Mtanzania kuperuzi kwa haraka zaidi,” alisema Baba Levo.
Amesema Kupitia TTCL Watanzania watajua nafuu iliyopo katika vifurushi pamoja na Data ambpo kazi hiyo ataifanya kwa weledi mkubwa kuitangaza.
Social Plugin