Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA WAPEWA MBINU KUTAMBUA FEDHA HALALI


Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa wamejifunza kwa vitendo jinsi ya kutambua fedha halali, ikiwa ni pamoja na alama za noti halali na jinsi ya kutunza fedha hizo, wakati Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilipotoa semina kuhusu majukumu ya benki hiyo na masuala ya kifedha.

Semina hiyo ya siku mbili, iliyoanza Novemba 14 hadi 15, 2024, imewahusisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mara, na Geita. 

Lengo kuu la semina ni kukuza uelewa wa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania, ili waweze kuandika habari na makala kwa usahihi na kuelewa vyema masuala ya uchumi na fedha.


Soma pia


BENKI KUU YA TANZANIA YATOA DAWA YA KUDHIBITI MIKOPO UMIZA
Waandishi wa habari kutoka Kanda ya Ziwa wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kutambua fedha halali, ikiwa ni pamoja na alama za noti halali na jinsi ya kutunza fedha hizo, wakati Benki Kuu ya Tanzania (BOT) - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com