Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BASHUNGWA AKABIDHI WAKANDARASI UJENZI MADARAJA MANNE - USHETU, BILIONI 18 KUTUMIKA

 

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Ushetu katika Kijiji cha Bugomba

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa (katikati)akiwa katika ziara ya kukagua hatua maendeleo ujenzi wa Madaraja Halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa ziara ya kukagua hatua maendeleo ujenzi wa Madaraja Halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga.

****

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametambulisha na kuwakabidhi Wakandarasi Wazawa kutoka Kampuni ya Salum Motors na Jonta Investment kwa Wananchi watakaoanza ujenzi wa madaraja makubwa manne ya Ubagwe, Kasenga, Ng’hwande na Mwabomba yaliyoathiriwa na mvua za El Nino katika Halmashauri ya Ushetu yatakayogharimu Shilingi Bilioni 18.05.

Aidha, Bashungwa ameuagiza Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga kuwasimamia Wakandarasi hao ili ujenzi wa madaraja hayo ukamilike kwa wakati na viwango vya ubora ili yaweze kutumika katika vipindi vyote.

Hafla hiyo ya kuwakabidhi Wakandarasi imefanyika leo Novemba 30, 2024 katika kijiji cha Bugomba A, Kata ya Ulewe katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga ambapo Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa madaraja hayo ukikamilika utaondoa changamoto na adha ya wananchi waliyokuwa wakiipata ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara misimu ya mvua kila mara.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza na kutupa fedha hizi ili kujenga madaraja yenye ubora na viwango ili miaka ya mbeleni tutakapokuja kujenga lami katika maeneo hayo, madaraja haya haya yatakuwa na ubora wa kuweza kubeba lami hiyo”, amesisitiza Bashungwa.

Kadhalika, Bashungwa ametoa wiki moja kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita kumkabidhi Mkandarasi eneo la mradi wa ujenzi wa daraja la Mwabomba (mita 50) ambalo linaunganisha Halmashauri ya Ushetu na Mkoa wa Geita.

Vilevile, Bashungwa amebainisha kuwa tayari  Wizara ya Ujenzi imeipandisha hadhi barabara ya Masumbwe - Mwambomba- Bugomba A - Igombe River (Km 124) kutoka Wilaya na kuwa ya Mkoa ili iweze kuhudumiwa na TANROADS na hivyo kufanya fedha za matengenezo ya barabara katika Jimbo la Ushetu kuongezeka kutoka Bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2023/24 hadi kufikia Bilioni 2.7 kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amewataka wananchi kuwa walinzi wa vifaa vya ujenzi pindi miradi hiyo inapotekelezwa kwa kutojihusisha na wizi wa mafuta, nondo na saruji na kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pindi watakapoona uhujumu wowote wa vifaa vya ujenzi.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Lutengano Mwandambo ameeleza ujenzi wa Daraja la Ubagwe (m 40) unagharimu Bilioni 4.14, Daraja la Kasenga (m 60) unagharimu Bilioni 5.13, Daraja la Ng’hwande (m 40) unagharimu billion 4.28 na Daraja la  Mwabomba (m 50) unagharimu Bilioni 4.5 pamoja na ujenzi wa tuta la barabara (m 300) kwa kiwango cha changarawe katika kila daraja kwa muda wa mwaka mmoja (miezi 12).

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha utekelezaji wa madaraja hayo makubwa ambayo yalipata madhara makubwa na kusababisha wananchi kukosa mawasiliano ya barabara na kukwamisha shughuli za usafiri na usafirishaji wa wananchi na mazao.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Samweli Mwambungu akitoa taarifa ya ujenzi wa Madaraja Ushetu.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Ushetu katika Kijiji cha Bugomba.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Ushetu katika Kijiji cha Bugomba.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Ushetu katika Kijiji cha Bugomba.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Ushetu katika Kijiji cha Bugomba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza katika ziara hiyo.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akizungumza na Wakandarasi ambao wanajenga daraja la Ubagwe.
Daraja ambalo wanapita wananchi wa Ubagwe ambalo litafanyiwa ukarabati mkubwa na kuwa daraja la kudumu.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa wapili (katikati) akiwasili Bugomba Halmashauri ya Ushetu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com