Na Regina Ndumbaro - Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Ahmed Abbas Ahmed ameshiriki na wakazi wa Mkoa huo katika upigaji kura wa kuwapata Viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Mkuu huyo ameshiriki katika upigaji huo wa kura katika mtaa wa Mashujaa uliopo kata ya Mjini Manispaa ya Songea Mkoani humo.
Pia Wananchi wamejitokeza katika Mkoa huo kupiga kura ya kuwapata Viongozi watakaowatumikia kwenye maeneo yao.
Aidha kwa upande wa Wananchi wa kata ya Pachanne 'B' kata ya Lizaboni wamesema wamefika kwenye vituo vya kupigia kura na taratibu zote zipo vizuri .
Hamasa ya wakazi wa Mkoa huo juu ya upigaji kura mwamko inadaiwa kuwa ni mkubwa hivyo itapelekea kuwapata Viongozi wanaowataka.
Social Plugin