Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM KATA YA KILIMANI KUENDELEA KUKINADI CHAMA NYUMBA KWA NYUMBA




Na Mwandishi wetu, DODOMA

Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani kimeanza kupiga kampeni za nyumba kwa nyumba kitanda kwa kitanda shuka kwa shuka kwa lengo moja tu la kusaka kura kwa wagombea wao wanaopeperusha bendera ya CCM kuwania nafasi za wenyeviti wa mitaa yote minne na wajumbe wao watano katika kata ya Kilimani Jijini Dodoma.

Zoezi hili la kusaka kura za CCM la nyumba kwa nyumba limeanza baada ya kuzinduliwa kwa kampeni za vyama vya siasa Novembar 20 mwaka huu.

Katika mtaa wa chinyoyo,Nyerere na kilimani baadhi ya viongozi wa chama Cha Mapinduzi wa tawi la kilimani wameongozana na Mjumbe wa kamati ya siasa kata ya kilimani Comredi Barnabas kisengi pamoja na wagombea wao kwa nafasi za wenyeviti na wajumbe wao wamepita katika Mitaa ya Nyerere na kilimani kwenye nyumba kwa nyumba kuomba kura za wagombea wao siku ya Novembar 27 mwaka huu.

Ndugu Janet Chibago na Lussy Rutainurya ni wagombea wa nafasi ya wenyeviti wa mitaa ya Nyerere na kilimani wameongazana na jopo la viongozi wa CCM kata ya kilimani kwenye tukio hilo la kusaka kura za CCM siku ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya siasa kata ya kilimani Comredi Barnabas kisengi amesema lengo la kampeni hizo za nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda, shuka kwa shuka ni zoezi endelevu hadi siku ya Novembar 26 mwaka huu.

"Kampeni hii tutakwenda nayo hadi siku ya mwisho ya kupiga kampeni ambayo ni Novembar 26 mwaka huu tukiwa tunakumbushana tu kuhakikisha tunawachagua viongozi wetu wa mitaa yote minne wanaotokana na chama cha Mapinduzi"amesema Comredi kisengi

Aidha Mjumbe huyo amewasisitiza wanachama, wakereketwa wote wa CCM kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura huku pia akiwataka na go wanachi wote wa kata ya Kilimani waliojiandikisha kwenye daftari la wakazi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenda kuwachagua Viongozi wao kwani watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia na kikatiba kupata viongozi bora ambao wanatokana na chama cha Mapinduzi.

Comredi kisengi amesema zoezi hilo sasa linaendelea kwenye Mtaa wa chinyoyo na Image kuendelea kusaka kura hizo kwa kishindo kikubwa.

Kauli mbiu ya chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jiji Dodoma inasema ifikapo November 27 wanachama na wakereketwa na wananchi sote kwa pamoja tunakwenda kwenye jambo litu huku tukisema "TUNAPIGA TUKISHAPIGA HAKUNA WA KUTUPINGA" CCM ni mwanzo hadi mwisho hadi KIELEWEKE.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com