CCM YASAMBAZA VIONGOZI NA MAKADA WAANDAMIZI NCHI NZIMA


-Ni uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

-Katibu Mkuu Balozi Nchimbi kuongoza kampeni hizo

-Yaonesha umuhimu wa uchaguzi na dhamira ya kufikia wananchi moja kwa moja

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, anatarajiwa kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za CCM Mkoa wa Mwanza tarehe 20 Novemba 2024, akiongoza viongozi na makada wa CCM waliotumwa maeneo mbalimbali nchini kwa kazi hiyo.

Balozi Nchimbi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Mwanza, atazindua kampeni hizo katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Furahisha, Nyamagana, jijini Mwanza.

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambao ni walezi wa mikoa mingine, pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), wamepewa jukumu la kuzindua kampeni hizo katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa tarehe hiyo hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, atazindua kampeni Mkoa wa Mbeya, huku Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Mohamed Dimwa, akizindua kampeni Mkoa wa Katavi.

Viongozi wengine wa CCM waliopangiwa kuzindua kampeni ni pamoja na:

- *Ndugu Issa Haji Usi Gavu*, Katibu wa NEC - Oganaizesheni, mkoani Geita.

- *Ndugu Amos Gabriel Makalla*, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, mkoani Dar es Salaam.

- *Ndugu Rabia Himid Abdalla*, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, mkoani Kilimanjaro.

- *Mhe. Dkt. Isdory Phillip Mpango*, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Dodoma.

- *Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa*, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkoani Kigoma.

- *Mhe. Hemed Abdulla Suleiman*, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, mkoani Tanga.

- *Mhe. Zuber Ali Maulidi*, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mkoani Singida.


Viongozi wengine ni pamoja na:

- *Komredi Mary Pius Chatanda*, Mwenyekiti wa UWT Taifa, mkoani Arusha.

- *Ndugu Mizengo Kayanza Pinda*, Waziri Mkuu Mstaafu, mkoani Mtwara.

- *Ndugu Halima Mamuya*, mkoani Njombe.

- *Ndugu Nasir Ally Juma*, mkoani Tabora.

- *Ndugu Mohamed Aboud Mohamed*, mkoani Iringa.

- *Komredi Mohamed Ali Mohamed Kawaida*, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, mkoani Morogoro.

- *Ndugu Fadhili Maganya*, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, mkoani Simiyu.

- *Dkt. Dotto Mashaka Biteko*, Naibu Waziri Mkuu, mkoani Mara.

- *Ndugu Hussen Bashe*, mkoani Shinyanga.

- *Ndugu Livingstone Lusinde*, mkoani Manyara.

- *Ndugu Ally Hapi*, mkoani Kagera.

- *Ndugu Nape Nnauye*, mkoani Rukwa.

- *Ndugu Zainab Shomari*, mkoani Lindi.

- *Ndugu Salim Faraji Abri (Asasi)*, mkoani Ruvuma.

- ⁠Ndugu Jokate Mwengelo, mkoani Pwani.




- ⁠Richard Kasesela*, Mjumbe wa NEC, mkoani Songwe.

Mkakati huu wa kuzindua kampeni kwa mtindo wa ushirikiano wa karibu kati ya viongozi wakuu na wanachama unaonesha jinsi CCM inavyothamini uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Pia, unadhihirisha dhamira ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani, ambavyo hadi sasa vimeshindwa kusimamisha wagombea wa kutosha kushindana kikamilifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post