Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepata ushindi wa jumla wa wenyeviti wa vijiji kwa nafasi ya viti 12,150 sawa na asilimia 99.01 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikipata jumla ya viti 97 sawa na asilimia 0.79.
Mchengerwa amesema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.
"Chama cha ACT kimepata viti 11 sawa na asilimia 0.09, Chama cha CUF kimepata jumla ya viti 10 sawa na asilimia 0.08, NCCR Mageuzi imepata kiti kimoja sawa na asilimia 0.01" ameongeza Mchengerwa.
Social Plugin