Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPENI ZA UCHAGUZI ZAKOLEA SHINYANGA MJINI, BWANGA ATAKA USTAARABU


Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini kimewataka wagombea wote wa serikali za mitaa kufanya kampeni kwa njia ya kistaarabu ili kuhakikisha mikutano hiyo inafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. 

Rai hii imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Bwana Said Bwanga, katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika mtaa wa Viwandani, kata ya Mjini.

Bwanga aliwasisitiza wagombea wa chama hicho kutumia majukwaa ya kampeni kwa lengo la kutangaza sera zao kwa lugha ya kistaarabu, badala ya kutumia lugha zinazochochea chuki na kugawa wananchi. Alihimiza kuwa kampeni za kisiasa zinapaswa kuwa na mwelekeo wa kujenga na kuleta umoja katika jamii.

Aidha, mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa wa Viwandani, Ashiraf Majariwa, ambaye anataka kuchaguliwa kwa mara ya pili, amewahimiza wakazi wa mtaa huo kumwamini ili aweze kuendelea kushirikiana nao kutatua changamoto na kero zinazowakabili.

Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini wanaendelea kufanya kampeni zao, wakielezea sera zao na ahadi za kuboresha maisha ya wananchi.












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com