Julius Shedrack, aliyekuwa mgombea wa mtaa wa Viwandani katika kata ya Unga LTD jijini Arusha kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akimsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuendeleza taifa.
Julius ameonyesha kuguswa na kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia, hususan katika kuboresha miundombinu na sekta ya elimu, hasa mikopo ya elimu ya juu.
Akizungumza kuhusu uamuzi wake, Julius alisema, “Leo nimeamua kurudi nyumbani. Nina sababu chache, ikiwemo kuunga mkono juhudi za mama yetu Samia Suluhu Hassan. Kweli kabisa mama yetu anafanya kazi.”
Aidha, alieleza kuwa hata ndani ya CHADEMA, ingawa chama hicho hakimuungi mkono waziwazi Rais Samia, bado wanakiri kimyakimya maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wake.
Julius pia alikosoa CHADEMA, akidai kuwa chama hicho hakijafikia kiwango cha kupewa madaraka kutokana na changamoto zake za ndani na migogoro.
Social Plugin