Mwenyekiti wa UWT-Taifa Mary Chatanda akiteta jambo na Rosemary Senyamule Mkuu wa mkoa wa Dodoma leo November 1,2024 kwenye uzinduzi wa UWAWAMA.
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
Mwenyekiti wa UWT-Taifa Mary Chatanda amezindua Umoja wa Wanawake Wafanya biashara Mosoko yote Jijini Dodoma (UWAWAMA) huku akiwataka wanawake hao kuachana na mikopo yenye masharti magumu inayochangia kuanguka kiuchumi.
Pamoja na Mambo mengine uzinduzi huo umehudhuriwa na wanawake wa masoko mbalimbali kama soko la Ndugai, Sabasaba, Mahengo, Machinga na Bonanza. Pia na vikundi mbalimbali kama Wanawake na Samia, wanawake na Nyerere, (Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Dodoma Jiji (JUWAKIDO).
Akizungumza leo November 1,2024 kwenye Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Roma Complex ,Chatanda ameitaja mikopo hiyo iliyojizolea umaarufu kwa majina tofauti kulingana na maeneo husika ikiwa ni pamoja na Kausha damu, ujinga na mwendokasi kuwa inatumika kuwadhalilisha na kuwaangusha Wanawake.
Chatanda amewataka wanawake wafanyabiashara kuachana na mikopo hiyo na badala yake wajiunge kwenye vikundi ili kupata Mikopo ambayo inatolewa Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambayo ina masharti nafuu na kuwasaidia kufanya biashara yenye faida.
"Kopeni kwenye mikopo ya serikali, acheni hiyo mikopo inayowanyanyasa na kuwadhalikisha, mikopo hiyo muuda wake wa marejesho ni mfupi na kiwango cha riba kikubwa kwa lugha nyingine tunasema unakopa asubuhi laki alafu jioni unatakiwa kuirudisha na riba sasa hiyo faida unakuwa umeipata saa ngapi,!?"anahoji Mwenyekiti huyo wa UWT
Pamoja na hayo nafafanua kuwa, "Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia imerejesha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa utaratibu ulioboreshwa zaidi ikiwemo kutumia benki kwa Halmashauri 10 za majaribio ikiwemo za Dodoma",amesema
Mbali na hilo amewahimiza Wanawake nchini kuchangamkia fursa mbali mbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kushiriki kikamilifu zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ambao upo mbioni kufanyika.
"Nawashukuru wanawake wa nchi nzima kwa kuitikia wito wa kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAMISEMI inaonesha wanawake walioandikishwa ni alilimia 51.29 na asilimia 48.71 ni wanaume, "ameeleza
Kuhusu Mashamba ya Kilimo cha Mboga Mboga Chatanda amesema,
"Suala hili nimelipokea, ni
jambo jema suala la Serikali ya Mkoa kuona mnasaidiwa na kupata
ushauri kwa Waziri wa Kilimo,kupitia Mkutano huu naendelea kuziomba Halmashauri
kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanawapatia
Mafunzo ya elimu ya Ujasiriliamali kwa vikundi vyote vinavyoomba
mikopo kabla ya mikopo kutolewa ili pesa zinazopatikana zikatumike
kama iliyokusudiwa, "amesisitiza
Aidha amesema watoa mikopo wanapaswa kutoa kipaumbele kwa vikundi
vyenye sifa na watakaoonyesha nia thabiti katika kujijenga.