📍 20 Novemba, 2024 - Karatu Arusha
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Mary Pius Chatanda (MCC)* amewataka wanachama wa CCM kudumisha umoja na mshikamano ndani ya Chama ili kuweza kushinda kwa kishindo uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Chatanda ameyasema hayo hii leo aliposhiriki zoezi la Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Wilayani Karatu.
Chama Cha Mapinduzi ndiyo tumaini pekee Kwa Watanzania tunalojukumu kubwa la kuwa wamoja na Kuhakikisha Tunakwenda kupiga Kura ya NDIYO siku ya Tarehe 27 Novemba, 2024.
Ameyasema hayo Wakati akikabidhi Tamko la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa la Chama Cha Mapinduzi Kwa Wagombea wake, ambayo ndiyo mwongozo Kwa Wagombea wake.
Social Plugin