Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DCEA YANG’ARA TUZO ZA NBAA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeibuka kinara kwa kushika namba moja kwenye usimamizi wa fedha na kutunikiwa tuzo ya uandaaji bora wa hesabu kwa Mashirika ya umma kwa kufuata viwango vya kimataifa vya uandaaji hesabu (International Financial Reporting Standards - IFRS).

Tuzo hiyo ilipokelewa na Kamishna DCEA Hussein Mbaga akimwakilisha Kamishna Jenerali. Aretas Lyimo katika hafla hiyo iliyofanyika Jana Novemba 29,2024 katika kituo Cha wahasibu Bunju-Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya hafla hiyo, Kamishna Mbaga ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwakuiwezesha taasisi hy kifedha ambapo zimekuwa zikitumika kufanya kazi iyokusudiwa.

Aidha ameipongeza timu nzima ya Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwani kupitia uwajibikaji wao ndio umechagia kupatikana kwa ushindi huo.

Kwa upande wake,Muhasibu Mkuu DCEA,Steven Galatia amesema kuwa ushindi wao unatokana na kufuata maelekezo vizuri kutoka hazina wanapo pokea fedha na kuzitumia kwa kufuata misingi waliyopewa.

Aidha Galatia amewashukuru waandishi wa habari kwa kuunga mkono juhudi zao kwenye mapambano ya kudhibiti matumizi ya dawa hizo hatarishi katika afya ya binadamu ili kuendelea kuwa na kizazi chenye utu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com