Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA "THE WHEEL" YAFUNGUA KITUO CHAKE CHA KWANZA DODOMA KURAHISISHA HUDUMA KWA JAMII


Msemaji wa kampuni ya The Wheel inayohusu urekebishaji na utunzaji wa magari Chris Mendoza akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzindizi wa kampuni hiyo Jijini Dodoma November 30,2024

Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Kampuni ya Urekebishaji na Utunzaji wa magari ya The Wheel imefungua kituo chake cha saba cha utoaji huduma jijini Dodoma ambapo Kituo hicho kipya ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo kupanua huduma zake nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Amin Lakhani ameeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha huduma za urekebishaji wa magari zinapatikana kwa urahisi zaidi kwa wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani.

Akizungumza leo November 30,2024 kwenye uzinduzi wa kampuni hiyo, Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa, Dodoma ina nafasi nzuri ya kuwekeza kutokana na kuwa mji mkuu na hivyo kuwashauri wawekezaji wengine kuwekeza zaidi katika mji huu na kueleza kuwa kuwepo kwa huduma bora za magari kutachangia katika kukuza uchumi wa mji na taifa kwa ujumla.

" Kampuni ya The Wheel inatarajia kuwa kituo hiki kitatoa ajira kwa vijana na kusaidia kuimarisha miundombinu ya usafiri katika mji wa Dodoma,kwa ujumla leo tunafurahi kufungua kituo cha kwanza hapa Dodoma ambapo itakuwa ni Cha saba kwa Tanzania,Mtanzamo wetu unahusu ubora,usalama na uamunifu huku tukihakikisha Kila safari inakuwa kadri ya maono yetu, "Amesisitiza.
Lakhani amezungumzia umuhimu wa kufungua kituo hicho cha magari kuwa ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za usafiri na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi na kwamba kitasaidia kuleta manufaa kwa kuwapa huduma bora .

Amesema The Wheel inakusudia kupanua huduma zake katika maeneo mengine ya nchi, lengo likiwa ni kuhakikisha wanapatikana kwa urahisi na kuendelea kuchangia katika maendeleo ya sekta ya usafiri.

Kwa upande wake, msemaji kutoka kampuni hiyo ya urekebishaji na utunzaji wa magari Chris Mendoza, amesema uzinduzi wa teknolojia hiyo mpya utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya huduma za magari kwa mafundi.

Mendoza ameeleza kuwa teknolojia hiyo si tu itaokoa muda bali pia itaongeza usalama wa mafundi wanapofanya kazi zao na kufafanua kuwa kupitia teknolojia hiyo, mafundi watakuwa na uwezo wa kugundua matatizo ya magari kwa haraka zaidi, jambo ambalo litapunguza muda wa matengenezo na kuongeza ufanisi wa kazi.
Anafafanua kuwa,"Teknolojia hii mpya ni ya namna ya utengenezaji wa magari, hivyo ni fursa kubwa kwa mafundi kujifunza na kuboresha maarifa yao,teknolojia hii itahusisha vifaa vya kisasa vinavyotumia akili bandia (AI) na mifumo ya uchanganuzi wa data, jambo litakalorahisisha zaidi utambuzi wa hitilafu hata kabla ya kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa gari, "ameeleza.

Sambamba na hayo Msemaji huyo maeeleza matarajio ya Kampuni hiyo ni kuona mafundi wakifanya kazi kwa ufanisi mkubwa, wakipunguza makosa, na kuhakikisha magari yanarejeshwa kwa wateja katika hali bora zaidi na kwamba mafunzo ya mara kwa mara kwa mafundi yatawezesha waweze kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

"Ni muhimu kwa mafundi kufahamu jinsi ya kutumia mashine hizi mpya, kwani zinahitaji ujuzi maalum ambao unapaswa kufundishwa, kampuni hii itashirikiana na vyuo vya ufundi na taasisi za mafunzo ili kuhakikisha mafundi wanaopata mafunzo wanapata ujuzi unaohitajika kwenye soko la sasa, "ameeleza

Pamoja na mambo mengine Kampuni hiyo imejinasibu kuaminika kwa kutoa huduma za haraka za fitment na matengenezo ya magari na kueleza kuwa ina vifaa vya kisasa vilivyoyengenezwa kwa ubunifu mkubwa kwa lengo la kuongeza usalama barabarani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com