Watu 13 wamefariki Dunia kutokana na tukio la kuporomoka kwa jengo la Ghorofa katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam lililotokea Novemba 16, 2024.
Taarifa iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan imeeleza kuwa idadi hiyo ni hadi kufikia Novemba 17, 2024, Saa 4 Asubuhi huku Watu 26 wakiendelea na matibabu Hospitalini kati ya 84 waliookolewa
Pia, Rais amesema Serikali itabeba gharama za matibabu kwa waliojeruhiwa pamoja na mazishi ya waliofariki. Aidha, ametaka kupata taarifa ya Mmiliki wa Jengo kuhusu ujenzi uliokuwa ukiendelea hadi kutokea tukio hilo.
Social Plugin