Kazi iendelee hiyo ndio Kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Utimilivu wa dhamira hiyo umeonekana mkoani Kigoma, ambako wametengewa Bilioni 46.3 kwa ajili ya kuboresha Miundombinu ya Miji ya Tanzania chini ya mradi wa TACTIC.
Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Zainab Katimba ameieleza dhamira hiyo ya Rais Samia wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu la Mwanga na Soko la Samaki la Katonga yaliyopo katika Manispaa ya Kigoma.
Katimba amesema kwamba miradi hiyo itajumuisha mradi wa ujenzi wa barabara zenye urefu Km. 9.51 na mitaro ya maji ya mvua yenye jumla ya urefu wa Km. 5.4 ambayo ujenzi wake unaendelea.
Amesema mkataba wa ujenzi wa Soko Kuu katika eneo la Mwanga na Soko la Samaki katika eneo la Katonga ambao utagharimu shilingi bilioni 16.5.
“Ni matarajio yetu sote kuwa miradi hii italeta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na wageni mbalimbali ambao watanufaika na huduma za mahitaji mbalimbali ya vyakula na mavazi pamoja na mazingira bora ya kibiashara”.
Ameongeza kusema kwamba miradi hiyo pia itaongeza thamani ya maeneo husika na hivyo kusababisha ongezeko la mapato kwa Halmashauri zote ndani ya Mkoa wa Kigoma.
Social Plugin