KONGOLE EWURA UTEKELEZAJI MKAKATI WA NISHATI SAFI KWA VITENDO





Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio,akizungumza na wafanyakazi wa EWURA wakati wa kikao cha Tatu cha Baraza kilichofanyika mkoani Morogoro, leo 11 Novemba 2024

*Na Mwandishi Wetu-MOROGORO

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepongezwa kwa kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia kwa vitendo kwa kuweka mfumo wa huduma hiyo katika shule ya Sekondari Morogoro na Kituo cha Makazi ya Wazee cha Fungafunga mkoani Morogoro.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt James Mataragio wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa EWURA kwa niaba ya Dkt. Biteko.

Pamoja na kufungua kikao cha baraza, Pia Dkt. Matarajio alizindua mradi wa nishati safi na salama ya kupikia katika Shule ya sekondari Morogoro, uliotekelezwa na EWURA, leo 11 Novemba 2024.

“Napenda kuwapongeza EWURA, wamekuja na jambo tofauti, ambalo lina matokeo Chanya na tija kwa jamii, sio kufanya tu kikao cha baraza kama vikao vingine, bali kugusa maisha ya watu, jambo hili litekelezwe na taasisi zote zilizo chini ya Wizara yetu,” alisema Dkt. Matarajio.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile akitoa taarifa ya mradi huo, alisema ni utaratibu wa EWURA kurudisha kwa jamii kwa namna mbalimbali na kwamba, mradi huo utasaidia wanafunzi zaidi ya 700 wa Shule ya Sekondari Morogoro na Wazee zaidi ya 104 katika makazi yao Fungafunga.

“Tunaahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya gesi ya kupikia kwa wapishi, walimu, wanafunzi na wasimamizi wa makazi ya wazee” alieleza.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Morogoro, Bonifasi Werema, alitoa shukrani kwa kupatiwa mradi huo ambao ameeleza utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi, walimu na wapishi, kutunza mazingira na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zikitumika kununua kuni.

Bi Rehema Kombe, Mfawidhi wa Makazi ya Wazee cha Fungafunga, alieleza kufurahishwa kwake na mradi huo, ambao ameeleza utaokoa mud wa kuandaa chakula kutoka saa tatu hadi dakika 45 na kupunguza gharama za kuni.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt James Andilile, akitoa taarifa ya mradi wa nishati safi na salama ya kupikia katika viwanja vya shule ya Sekondari Morogoro ambao umedhaminiwa na EWURA, leo 11 Novemba 2024.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt James Mataragio akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa nishati safi na salama wa kupikia katika shule ya Sekondari Morogoro, leo, 11 Novemba 2024



Dkt James Mataragio, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, akizungumza na wafanyakazi wa EWURA wakati wa kikao cha Tatu cha Baraza kilichofanyika mkoani Morogoro, leo 11 Novemba 2024



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt James Mataragio (katikati) Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Herman Tesha(kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, mjini Morogoro leo 11/11/24



Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Morogoro wakati wa uzinduzi wa mradi wa nishati safi na salama ya kupikia uliozinduliwa shuleni hapo ili kuwawezesha kupika kwa kutumia gesi badala ya mkaa, leo 11 Novemba 2024



Mkuu wa Shule ya Sekondari Morogoro Boniface Werema akitoa shukrani kwa kupatiwa mfumo unaowezesha kupikia nishati safi na salama leo 11 Novemba 2024.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt James Andilile(kushoto) akizindua mradi wa nishati safi na salama ya kupikia, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Mashaka Biteko(Mb),katika shule ya Sekondari Morogoro leo Novemba 2024. Kulia ni Dkt James Andilile, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA. Mradi huo wenye thamani ya milioni 40, umewezeshwa na EWURA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post