Na Mwandishi - Wetu Malunde 1 blog
Kijana aitwaye Raphael John (20) amefariki dunia baada ya kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikitokea mkoani Tabora kuelekea jijini Mwanza.
Ajali hiyo imetokea jioni ya leo Novemba 01, 2024 katika eneo la soko la Ibinzamata manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mashuhuda wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mara baada ya mtu huyo kukwama na pikipiki kwenye njia ya treni akitaka kuvuka huku treni ikipita.
Baadhi ya wakazi na wafanyabiashara wa soko la Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kujenga kivuko (daraja la juu) kwa ajili ya watembea kwa miguu wanaokwenda kupata huduma kwenye soko hilo ili kupunguza matukio ya ajali kwenye eneo hilo.
Jitihada za kuzitafuta mamlaka husika zinaendelea ili kupata undani wa tukio hilo.
Social Plugin