Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Paul Sangawe ameongoza Kikao cha Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), wakurugenzi wa sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na timu ya wataalamu.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho pia kimehusu mapitio ya Mipango na Bajeti ya Programu kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji iliyobakia.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 18 Novemba 2024 Zanzibar, katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi.
Social Plugin