Katika ziara hiyo viongozi hao walitembelea wateja wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na kuzungumza nao kuweza kujua namna wanavyozipokea huduma za MSD na kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha huduma hizo.
Akizungumza baada ya ziara hiyo mjumbe huyo wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dr. Magesa amesema kuwa wameweza kutembelea ghala la kanda ya Mkoa wa Mbeya na kujionea jinsi shughuli za ugavi wa bidhaa za afya zinavyofanyika.
Dr. Magesa ameeleza kuwa, amefurahishwa na ari ya watumishi wa MSD kanda ya Mbeya na utendaji wao ambapo umeonyesha kiwango cha juu cha juhudi na weledi.
Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru MSD kwa huduma bora wanazotoa na ushirikiano wa karibu ambao umesaidia hospitali hiyo kupata bidhaa za afya kwa wakati zikiwa na ubora unaostahili.
Naye Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya, Petro Mdegela, amesema ziara hiyo pia itahusisha kituo cha afya na zahanati ili kuweza kupata mrejesho wa huduma zinazotolewa na MSD katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za afya.
Social Plugin