Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MONGELLA AHITIMISHA KAMPENI ZA CCM SHINYANGA 'KACHAGUENI WAGOMBEA CCM, MSIVAE SARE ZA VYAMA'

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella, amewashauri wananchi kutovaa sare na nguo zenye rangi ya chama wakati wa kwenda kupiga kura za kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa kwenye maeneo yao.

Mongella amesema hayo leo Jumanne Novemba 26,2024 wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, mkutano uliofanyika katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga mkoani humo.

Mongella amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa wanaotokana na CCM ili waweze kuendeleza utekelezaji wa ilani ya chama hicho ulio tekelezwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika kesho Novemba 27 katika maeneo yate nchini kuwachagua Wenyeviti wa Vijiji Mitaa, Vitongoji,pamoja na wajumbe katika maeneo yao.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi akiwaombea kura wagombea amesema kuwa serikali imetoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Shinyanga katika sekta ya Afya ,Elimu ,Maji na Barabara.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella akihitimisha kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella akihitimisha kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara John Mongella akihitimisha kampeni za CCM Mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga Richard Masele akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Mkombe akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwa nadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Diwani wa Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella,akipokelewa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com