Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI UMMY AWASHUKURU RED CROSS NA TPA KWA MISAADA YA VIFAA SAIDIZI MAAFA KARIAKOO

 



NA. MWANDISHI WETU


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga amewashukuru wadau kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa kutoa misaada ya vifaa saidizi kwa ajili ya kuendelea kusaidia katika zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia janga la kuporomoka jengo la ghorofa eneo la Congo na Mchikichi Kariakoo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.


Ametoa shukrani hizo hii leo Novemba 19, 2024 na kueleza kuwa miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na machela tisa (9) mashuka 100 kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) Pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA, reflectors pamoja na  cover white.


Naibu Waziri huyo ameendelea kutoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia huku akipongeza namna zoezi la uokoaji linavyoendelea kwa kushirikiana na wadau.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com