NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya PPPC yamefanyika leo Novemba 11, 2024 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na umuhimu wa kutumia PPP katika utekelezaji wa Mipango ya Taifa ya Maendeleo ya nchi, muundo wa kisheria na Kitaasisi katika utekelezaji wa program ya PPP Tanzania, dhana ya PPP na Orodha ya Miradi ya PPP iliyoandaliwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Social Plugin