Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PPRA YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA MFUMO WA NeST


Mkurugenzi Mkuu wa MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba, akizungumza katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa vyombo ya habari nchini, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR). Kilichofanyika leo Novemba 4,2024 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Kanda ya Pwani wa PPRA , Vicky Mollel akizungumza katika kikao hicho kilifanyoka leo Novemba 4, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilisiano na Elimu kwa umma Serikalini,Ofisi ya Msajili wa Hazina - TR- Bw. Daudi Kosuri, akifafanua jambo alipouwa akitoa salami za utanguizi katika kikao hicho. 

Na; Hughes Dugilo, DAR

Mkurugenzi Mkuu wa MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba, amesema,kuwa katika kipindi cha mwaka 2023/24 wazabuni zaidi ya 28,590 wamejisajili kwenye Mfumo wa NeST huku mikataba ya zabuni 62,267 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10.2 ikitolewa kwa wazabuni mbalimbali kupitia Mfumo huo, nakwamba Serikali imeongeza bajeti ya ununuzi ya zaidi ya shilingi trilioni 38.6 kupitia Mfumo wa NeST, kama fursa ya wazi kwa ajili ya wazabuni.

Simba ameyasema hayo katika kikao kazi na wahariri na waandishi wa vyombo ya habari nchini, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR). Kilichofanyika leo Novemba 4,2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia mfumo huo wazabuni zaidi ya 28,590 wamejisajili huku mikataba ya zabuni 62,267 yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 10.2 imetolewa nakwamba hadi kufikia Oktoba 31, 2024 jumla ya taasisi za ununuzi 21,851 zimesajiliwa na zinatumia Mfumo wa Kielektroniki (NeST).

"ununuzi wa umma ni shughuli muhimu ya kiuchumi inayohusisha sehemu kubwa ya Pato la Taifa (GDP) takribani asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali na taasisi zake hutumika kwenye ununuzi wa umma, hivyo ununuzi wa umma nchini unasimamiwa na Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410." "Chini ya sheria hii zimeundwa Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2024 na miongozo kwa ajili ya kuweka taratibu za ununuzi wa umma. Kanuni mpya za Ununuzi wa Umma zimekwishakamilika." amesema Simba.

Pia amesema kuwa Mamlaka hiyo imewezesha ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma na kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kuanzisha kanda sita katika mikoa ya Mwanza, Dar es Saalam, Arusha, Mbeya,Tabora na Mtwara.

Ameongeza kuwa zabuni zenye thamani isiyozidi shilingi bilioni 50 zimetengwa kwa ajili ya wazabuni wa ndani ya nchi pekee nakwamba mumo wa NeST unaisaidia PPRA katika kulisimamia hilo kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari kufungua akaunti ya mfumo wa NeST ili kuweza kupata matangazo.

“Tuwapongeze kwa kurahisisha mfumo wa ununuzi katika nchi yetu, ndugu zangu wahariri, hata matangazo ya kwenye vyombo vya habari mengi yanapitia NeST, kwa hiyo sisi tunaoendesha vyombo vya habari kama huna akaunti ya NeST huwezi kufanikisha matangazo, hali ngumu ya vyombo vya habari tuliyonayo tuna nafasi ya kujikomboa kupitia kwenye mfumo huu” amesesema Bw. Balile.

PICHA ZA WAHARIRI KATIKA MKUTANO HUO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com