Rais wa Somalia, Mhe. Hassan Sheikh Mahmud amewasili nchini leo tarehe 29 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Rais Mahmud amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi umetanguliwa nab Kikao cha Ngazi ya Juu kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye kaulimbiu isemayo "Miaka 25 ya EAC: Tafakari ya tulikotoka na matarajio ya tunapokwenda"
Social Plugin