Uamuzi huo unatokana na nia ya serikali ya kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu nchini.
Ikumbuke kuwa tangu Juni, 2021 na Februari 2024, kumekuwa na malalamiko ya uhaba wa waalimu.
Walimu hawa wameelekezwa kwenda kutoa huduma kwenye shule mbalimbali nchini, na ujio wao unatajwa kusaidia kupunguza uhaba wa waalimu nchini.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs), ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa walimu kwa mwaka 2024.
Aidha nafasi 600 za ajira za walimu zilikuwa ni Daraja la III B kwa mwaka 2024, ambazo zilitangazwa na kuwekwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) na Idara mbalimbali za Serikali Kuu (MDAs) kote nchini na zilitolewa kama sehemu ya mpango wa serikali wa kuboresha sekta ya elimu kwa kuongeza idadi ya walimu wenye sifa ili kuboresha utoaji wa elimu bora nchini.
Mwaka 2020/21 hadi mwaka 2022/23, serikali iliweza kuajiri walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati 10,853.
Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi kirefu sasa serikali imekuwa katika mchakato wa kuhakikisha inaongeza idadi ya walimu katika shule za msingi na sekondari na Serikali ya awamu ya Sita imelipa kipaumbele.
#KAZIINAONGEA
Social Plugin