Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir akimpa mkono wa Heri Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Novemba 30, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024
..............
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir amewasili nchini leo tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)Mhe. Salva Kiir amepokelewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.)
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi umetanguliwa na Kikao cha Ngazi ya Juu kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye kaulimbiu isemayo "Miaka 25 ya EAC: Tafakari ya tulikotoka na matarajio ya tunapokwenda"
.
Social Plugin