Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameongoza sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Msimu wa Nne, ikiwa na lengo la kutambua na kupongeza michango ya wadau shupavu wa Manispaa ya Kahama, Halmashauri ya Msalala, na Ushetu.
Sherehe hii imefanyika usiku wa Novemba 3-4, 2024, katika ukumbi wa kifahari wa Zakaria (Miligo Hall) Mjini Kahama ambapo tuzo mbalimbali, ikiwemo za heshima, zimekabidhiwa kwa wadau shupavu 30, ambao ni mashirika, watu binafsi, na vikundi vilivyofanya kazi kubwa katika sekta za elimu, afya, miundombinu, biashara, na uwajibikaji wa kijamii (CSR).
Pia, majiko ya gesi yalitolewa kwa Mama Lishe, Baba Lishe, na makundi maalum.
Sherehe hiyo iliyoongozwa na MC Pilipili imejumuisha burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wachekeshaji Oscar Nyerere na Matabe ‘Nimekoma’, huku wadau wakishiriki chakula na vinywaji.
Katika hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amepongeza Taasisi ya Holysmile kwa kuandaa tukio hili, akisisitiza umuhimu wa kusherehekea na kutambua michango ya wadau walioleta mabadiliko makubwa katika jamii.
Aidha amewataka vijana kufanyakazi kwa bidii, kujitahidi kutafuta fursa za uwekezaji na kuwa wabunifu, akitoa mfano wa kijana Matabe anayeweza kujipatia kipato kupitia uchekeshaji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha.
"Nimemsikia Matabe akichekesha akitumia kauli mbiu ya 'Nimekoma!' Nami nasema, vijana komeni kuhangaika na mashangazi, acheni kukimbizana na mashangazi, bali tafuteni fursa za mahusiano mazuri na mtambue upo umuhimu wa kuwa na marafiki na kuwekeza muda katika uhusiano wa kijamii. Jitahidini kushiriki katika shughuli za maendeleo ya jamii",amesema Macha.
Macha pia amehimiza wananchi kudumisha amani na kutumia nishati safi, akisisitiza kuwa gesi na umeme ni muhimu kwa afya na mazingira.
“Nishati safi ni ajenda ya kitaifa, ni ajenda ya Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Gesi na umeme siyo anasa, tunataka nishati safi katika maisha yetu ya kila siku ili kulinda afya zetu pamoja na kutunza mazingira”,ameongeza Macha.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Mboni Mhita, amewakumbusha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Mratibu wa Wanawake kwenye Nishati ya Gesi, Bi. Winner Lukumay, amesisitiza umuhimu wa kuunga mkono ajenda ya serikali katika matumizi ya nishati safi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Burudani ya HolySmile, Anord Bweichum , ameshukuru washiriki wote kwa mapokeo mazuri na kueleza kwamba Usiku wa Mdau Shupavu ni tukio muhimu linalokusanya wadau wa maendeleo kutoka Halmashauri za Kahama, Ushetu, Msalala, na wilaya jirani.
Bweichum amebainisha mafanikio ya Taasisi ya HolySmile, ikiwa ni pamoja na kuanzisha jukwaa la sanaa ya uchekeshaji na matamasha ya utoaji tuzo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya HolySmile, Anord Bweichum
Amesema kuanzia mwaka 2024, watawakutanisha halmashauri zote tatu katika jukwaa moja la MDAU SHUPAVU AWARDS.
Hata hivyo amesema licha ya mafanikio, Taasisi ya Holysmile inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na upotoshaji wa taarifa kuhusu matamasha.
Bweichum amesisitiza umuhimu wa kila mmoja katika kuinua jamii na kuwakaribisha wadau wote kuendelea kuunga mkono juhudi hizi.
Bweichum amehimiza ushirikiano zaidi ili kufanikisha malengo ya maendeleo na kuwathibitishia wadau kwamba kila juhudi inachangia katika kujenga mustakabali mzuri wa jamii.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINIMkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akitoa hotuba wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Msimu wa Nne iliyofanyika Mjini Kahama Novemba 3/4,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Burudani ya HolySmile, Anord Bweichum akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Burudani ya HolySmile, Anord Bweichum akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Afisa Mahusiano Taasisi ya HolySmile, Hancelin Sunday akisoma risala wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Mchekeshaji maarufu Matabe ‘Nimekoma' akitoa burudani wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mchekeshaji maarufu Matabe ‘Nimekoma' akitoa burudani wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Mchekeshaji maarufu Oscar Nyerere akitoa burudani wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Mratibu wa Wanawake kwenye Nishati ya Gesi, Bi. Winner Lukumay akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mratibu wa Wanawake kwenye Nishati ya Gesi, Bi. Winner Lukumay akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Mratibu wa Wanawake kwenye Nishati ya Gesi, Bi. Winner Lukumay akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Msambazaji wa Gesi ya Oryx kutoka Kampuni ya Kagoli Enterprises, Kokusima Alex Kalokola akizungumza wakati Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
MC Pilipili akiongoza Sherehe maalum ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama
Keki Maalumu wakati wa Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Msimu wa Nne
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akikata keki Maalumu wakati wa Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za mdau Shupavu Wilaya ya Kahama Msimu wa Nne
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akikabidhi majiko ya Gesi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akikabidhi majiko ya Gesi kwa mamalishe na baba lishe
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akikabidhi majiko ya Gesi
Burudani ikiendelea
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akicheza muziki na wadau Shupavu
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akicheza muziki na wadau Shupavu
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akicheza muziki na wadau Shupavu
Wadau Shupavu wakicheza muziki
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akigawa tuzo za Heshima kwa Wadau Shupavu
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Wadau Shupavu wakiwa ukumbini
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com