SHEIKH WA DODOMA AAHIDI KUONGEZA BIDII KUITUMIKIA JAMII




Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Alhaj Mustafa Rajabu Shaban ametunukiwa Udaktari wa heshima(PhD)huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha heshima hiyo inaleta manufaa kwa jamii hususani kwa watu walioko kwenye mazingira magumu.

Aidha Shekhe Mustafa ni mmoja kati ya watunukiwa nane wa PhD ambao wamedhaminiwa na Chuo cha Outreach Care International kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornerstone International College cha USA, Lucent University cha uengeleza na HHWB College - USA

Akizungumza kwenye halfa ya kumpongeza hivi karibuni Jijini hapa amesema tunu hiyo sio sifa ya kujiona kuwa fahari mbele ya jamii bali itamchochea katika kuongeza uwajibikaji kwa kuitumikia jamii ikiwa ni pamoja na kuendelea kueneza mafundisho ya wema, heshima na kumtumikia Mungu kwa njia sahihi.

"Katika maisha yangu ya dini, nimedhamiria kila wakati kuwa mfano mzuri wa maadili, amani, na mshikamano,nimejizatiti katika kueneza ujumbe wa upendo, ushirikiano, na mshikamano kwa ajili ya amani ya nchi yetu,na hili ndilo lengo langu kila wakati kwa sababu tumetumwa kuitumikia jamii na kuongeza juhudi zaidi tofauti na tulivyofanya mwanzo, "amesema


Shekhe Mustafa pia amesema, "Nashukuru kwa fursa hii ya kipekee, ambapo leo hii nimepata heshima ya kutunukiwa udaktari wa heshima, ni heshima kubwa ambayo siwezi kuikwepa bila kumshukuru Mungu na kuwashukuru watu wote walioshirikiana nami katika safari yangu ya maisha, " amesema na kuongeza;

"Nawashukuru sana viongozi wa dini, viongozi wa Serikali, na wadau wengine wote ambao wamekuwa sehemu ya mafanikio yangu na mimi kuweza kuleta mchango wangu katika jamii yetu ya Dodoma na Tanzania kwa ujumla, " ameeleza

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Shekimweri ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ameeleza kuwa tunu hiyo ina mafundisho katika jamii kwamba penye nia na malengo, juhudi na dhamira ya dhati, Mungu hufanikisha.

Amesema kutunukiwa udaktari wa heshima siyo tu heshima binafsi, bali ni heshima ya jamii na wote waliokuwa na imani na juhudi katika kuleta mabadiliko chanya.

Shekimweri pia ametumia nafasi hiyo kumuomba Shekhe huyo kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia watu, kuhimiza mshikamano na amani, na kuhakikisha kwamba maadili yanaendelea kuwa mwanga kwa jamii .

Naye Mhadhiri wa masomo na msimamizi kwa njia ya mtandao Dkt .Kharid Salaa ametumia nafasi hiyo kuwashauri Wahitimu wa elimu ya vyuo vikuu mara wanapohitimu kutekeleza majukumu yao ya kazi na uongozi kwa ushirikiana na jamii inayowazunguka ikiwemo kuwafumdisha ujuzi walioupata ili kujenga Taifa






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post